Daniel Sturridge ataanza katika
kikosi cha taifa cha Uingereza kwa mara ya kwanza tangu kupita miezi
18 wakati wakiikaribisha Uholanzi katika dimba la Wembley hii leo.
Mshambuliaji huyo wa timu ya
Liverpool, amekosa michezo yote ya kuwania kufuzu michuano ya Euro
2016 kutokana na kuwa majeruhi.
Kocha Roy Hodgson anatarajia kufanya
mabadiliko ya kikosi kilichocheza jumamosi na kushinda mabao 3-2
dhidi ya Ujerumani, huku kipa Fraser Forster akitarajia kuwa langoni
hii leo.
Daniel Sturridge akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Uingereza
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni