Jumanne, 29 Machi 2016
TUNAITAJI UKUMBI BORA WA MCHEZO WA MASUMBWI TANZANIA
NDONDI ni miongoni mwa michezo maarufu mno hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.
Wapo wanamichezo waliojipatia heshima kubwa duniani kutokana na kufanikiwa kupitia mchezo wa ndondi.
Miongoni mwa wanamichezo hao ni nguli Mohammed Ali, Mike ‘Iron’ Tyson, Evender Holyfield, Floyd Mayweather, Manny Pacquiao na wengineo wengi.
Mchezo wa ngumi katika nchi yetu ya Tanzania unazidi kushika kasi kutokana na kuchipukia kwa mabondia wengi na mapromota ambao wanapigana katika kuwania mataji mbalimbali nje na ndani ya Tanzania na kuandaa mapambano.
Wapo mabondia wengi katika historia ya Tanzania ambao wamewahi kupigana nje ya nchi, ukiwauliza kuhusu ubora wa mchezo wa ngumi katika upande wa vifaa vya mchezo huo ndani ya nchi yetu ni imani yangu waliowengi wanaweza kukubaliana nami kuwa bado unahitaji vitu muhimu ili kuendeleza mchezo huo .
Kwa Tanzania tumekuwa na mabondia wengi ambao wameweza kutingisha nje ya Tanzania kama Stanley Mabesi 'Ninja' Joseph Marwa, Rashid Matumla, Rogers mtagwa ,Habibu Kinyogoli Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi na ni mwanaharakati wa mchezo huo kwa nyanja zote kwa sasa na Emanuel Mlundwa ambao waliweza kutwaa mataji mbalimbali ya mchezo huo.
Jambo moja kuu ambalo watanzania tunalisahau ni kukosekana kwa kumbi bora ya mchezo huo kwa upande mwingine kuna wakati baadhi ya watu wanaohusika na mchezo wa ngumi waliwahi kuwa na wazo hilo lakini nimeona nijaribu kulitilia mkazo .
Natoa mfano kama tulivyoweza kujenga uwanja wa taifa na kuziona nchi kubwa duniani zikija kucheza mechi za kirafiki kama Brazil, Ivory Coast na nyingine, basi hata mchezo wa ngumi linawezekana ukitazama kama Marekani ambao mchezo huu umekuwa kwa kiwango cha juu kutokana nchi hiyo kuboresha maeneo ya kuchezea, kumbuka silinganishi kiwango cha mchezo bali ni namna ya kuboresha.
Kwa Tanzania vipo vyama vingi vya mchezo wa ngumi PST,TPBC,TPBO,KBF bila kusahau kile cha taifa cha BFT lakini ni mara kadhaa Makore Mashaga katibu mkuu wa BFT amekuwa akizungumzia juu ya ukosefu wa vifaa maeneo ya mazoezi na kumbi za kupigania vimekuwa ni vikwazo vikubwa kwa mchezo huo kwa Tanzania kwakuwa serikali imeweza kuleta uwanja mpya wa mpira wa miguu ambao hata mchezo wa kufukuza upepo Riada wanafaidika nao halikadharika wanamuziki kupata studio ya kisasa ya kurekodia muziki bila shaka mchezo wa ngumi nao unahitaji eneo zuri la kuchezea mchezo huo kama ilivyo Las Vegas Nevada na MGM Grand au Madson square ni dhahiri inawezakana kwa Tanzania kuwa na kumbi bora ya kisasa na imani vyama vya mchezo wa ngumi vyote nchini vinaweza kukaa chini na kujadiliana na serikali kupitia wizara ya habari utamaduni na michezo kuhakikisha tunapata kumbi bora ya kisasa ya kupigania ili kuongezea ujuzi na viwango vya mchezo wa ngumi kwa Tanzania.
Kama Ufilipino imeweza kutoa bingwa wa dunia hata Tanzania inaweza pia kwani ukiacha soka mchezo wa ngumi ndio mchezo pekee ambao unakuja kwa kasi pengine liwe ombi rasmi kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Nina maliza kwa kusema kuwa ni imani yangu kuwa kwa kujengwa uwanja huo kutawapa mabondia wa tanzania kujiaamini na kuupanua mchezo huo na unaweza pia kulitangaza jina la Tanzania katika Nyanja za utalii ndani na nje ya Tanzania kama inavyowezekana kuleta mastaa wakubwa wa muziki kutoka ulaya na amerika ni dhahiri hakuna lisilowekana kwa Tanzania .
Lakini ikumbukwe kuwa ndondi ndio mchezo uliotoa mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwa sasa ambaye si mwingine bali ni Floyd Mayweather, akifuatiwa na Manny Paquaio mwanasoka raia wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo.
Anayeshika nafasi ya tatu ni mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James, wakati mwanasoka anayechezea Barcelona ya Hispania, Muargentina Lionel Messi akishika nafasi ya tano,
nina mengi ya kuongelea kuhusu mchezo wa masumbwi hila kwa leo naomba nishie hapo
Na: Super D Boxing Coach www.superdboxingcoach.blogspot.com Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni