Mshambuliaji wa Leicester, Shinji Okazaki akikimbia kwa furaha baada ya kufunga bao muhimu lililoisaidia timu yake kupata pointi tatu dhidi ya Newcastle United.
Timu hizo zilikutana jana usiku katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza, ambapo Leicester waliibuka na ushindi wa bao 1-0, na kwa matokeo hayo Leicester imeendelea kujiimarisha kileleni kwa kufikisha jumla ya pointi 63 na kuendelea kuwapa matumaini mashabiki wake kuwa itatwaa ubingwa msimu huu.
Mlinda mlango wa Newcastle akiruka bila mafanikio kujaribu kuzuia mpira uliojaa wavuni.Kocha mpya wa Newcastle, Rafa Benitez huu ukiwa ni mchezo wake wa kwanza akishuhudia jahazi likiendelea kuzama kwa timu hiyo ambayo ipo katika hatari ya kuteremka daraja. Newcastle niya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi 24.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni