Mshambuliaji wa Chelsea, Diego
Costa, amefunguliwa mashtaka ya utovu wa nidhamu baada ya kupata kadi
nyekundu katika mchezo na Everton jumamosi.
Mhispania huyo alitolewa nje baada
ya kugombana na kiungo Gareth Barry wa Everton katika dakika ya 84,
ambapo Chelsea ilifungwa mabao 2-0 katika dimba la Goodison Park.
Costa, 27, alionekana kama
anamng'ata Barry katika tukio hilo ingawa wachezaji wote wawili
wamekanusha kutokea tukio hilo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni