Maafisa wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Kusini Pemba, wakisubiri usafiri wa kuvukia kwelekea kisiwa Panza, kusikiliza matatizo ya wananchi yaliyopelekea kutokuvuushwa kwa baadhi ya wananchi wanaishi kisiwa hicho.
Viongozi mbali mbali wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa kusini Pemba, wa kiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla wakiwasili katika kisiwa Panza kwa boti ya Kikosi cha KMKM.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla akiwa katika harakati za kutaka kushuka katika faiba ya KM KM baada ya kuwasili katika kisiwa Panza kutoka Chokocho, kwa lengo la kuja kutatua mzozo uliopelekea baadhi ya wananchi kutokuvuushwa kwa madai ya kisiasa
Wananchi wa Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkao kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdall, wakati alipokuwa akizungumza nao kufuatia baadhi ya wananchi kukataliwa kuvushwa kisiwani huko kwa madai ya itikadi za kisiasa
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba Mhe: Mwanajuma Majid Abdalla akiwa na viongozi mbali mbali wa serikali katika kisiwa Pemba, kwa lengo la kukagua mazingira ya kisiwa hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba, wakati walipowasili katika kisiwa Panza kusikiliza matatizo yaliyopelekea baadhi ya wananchi kutokuvuushwa kwa madai ya kisiasa.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni