pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Wanawake mkoa wa Mwanza Mh. Zawadi Kiteto (Kushoto), wakati wa utekelezaji wa mradi wa kugawa taulo za usafi kwa Mabintiwa Shule ya Msingi Igombe.
Katika kusheherekea siku ya Wanawake Duniani Machi 08,2016, taasisi ya
kusaidia wanawake na wasichana yenye makao makuu jijini Mwanza,
DidaVitengeWear Foundation, Imefanikisha kugawa taulo za usafi zaidi ya
2,000 kwa wasichana zaidi ya 600 wa shule ya msingi Igombe na Shule ya
Sekondari ya Luchelele zote za Jijini Mwanza kupitia mradi wa kuwasaidia
Mabinti kufikia malengo yao, ujulikanao kama ‘Binti Box’.
Hatua hiyo pia imefikiwa kwa ushirikiano wa karibu baina ya taasisi hiyo pamoja na Mtandao wa Wanawake jijini Mwanza wa ‘Women Roundtable’, na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) Mh.Stanslaus Mabula, Mbunge Viti Maalum Wanawake Mkoani Mwanza Zawadi Kiteto na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Mkoani Mwanza Mh.Maria Kangoye Ndila.
Hatua hiyo pia imefikiwa kwa ushirikiano wa karibu baina ya taasisi hiyo pamoja na Mtandao wa Wanawake jijini Mwanza wa ‘Women Roundtable’, na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) Mh.Stanslaus Mabula, Mbunge Viti Maalum Wanawake Mkoani Mwanza Zawadi Kiteto na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Mkoani Mwanza Mh.Maria Kangoye Ndila.
Binti Box ni mradi ulioanzishwa kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike
waliopevuka kubaki shule na kuimarisha mahudhuria ya wasichana shuleni
kwa kuwapatia vifaa vya usafi vitakavyowasaidia wakati wa siku zao za
hedhi. Wasichana wengi hasa wa vijijini hukosa kwenda shule kwa siku 5
mpaka 7 kwa mwezi kwa sababu ya kukosa vifaa vya usafi wakati wa
mzunguko wa hedhi, hivyo mradi huu kwa upande wa kanda ya ziwa ni
mkombozi kwa mabinti wengi kuhudhuria shule na kuinua kiwango cha ufaulu
katika masomo yao.
Akiongea wakati wa kugawa taulo hizo za usafi mashuleni, Bi. Khadija
Liganga, Mratibu wa Mradi na Mkurugenzi wa DidaVitengeWear Foundation,
alieleza kwamba, elimu ya wasichana ni jambo la msingi katika jitihada
za kuleta maendeleo kwa nchi masikini kwa sababu mafaniko ya wanawake
hasa katika elimu inamaanika kuwa na faida ya muda mrefu na huenda mbali
Zaidi katika kuinua uchumi wa jamii na nchi.
“Kuna sababu nyingi zinazochangia kudumaa kwa ustawi wa elimu ya mtoto
wa kike hasa wale wa vijijini, tatizo la ukosefu wa vifaa vya usafi kwa
mabinti wakati wa hedhi kwa kila mwezi nayo imeibuka kuwa ni tatizo sugu
linalofumbiwa macho na wadau wengi wa maendeleo katika nchi
zinazoendelea na Tanzania ikiwemo.
Wasichana hawa hujawa na uwoga na
kuhofia kupoteza thamani yao na utu wao wawapo shuleni au mbele za watu
na kuwafanya wasihudhurie darasani au kutokwenda shule na matokeo yake
wengi huacha shule,” amesema Bi. Khadija Liganga.
Bi.Khadija aliendelea kusema kwamba “Baada ya kutembelea baadhi ya shule
zilizo pembezoni na miji tumegundua tatizo ni kubwa, tukapata uwelewa
wa kutosha na tukaona ni vyema badala ya kuandaa makongamano ya wanawake
wakati wa sherehe za Siku ya Wanawake Dunaini 2016, kwanini tusiguse
eneo ambalo ndio chimbuko la ukandamizaji wa maendeleo ya Mwanamke,
ambalo ni Elimu.
Ndipo tukaja na huu mradi utakaokuwa endelevu wa ‘Binti
Box’ kwa lengo la kutoa taulo za usafi kwa mabinti wa shule za msingi
na sekondari pamoja na elimu ya usafi wakati wa siku za hedhi.
“Tungependa kuwashukuru watu wote pamoja na taasisi mbalimbali kwa
mchango wa o wa maboksi ya taulo za usafi. Huu ni mwanzo tu, huku
mipango ikiwa ni kuongeza uwezo wa mradi kuweza kutoa huduma hii kwa
shule za sekondari na msingi katika mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, tuko
tayari kushirikiana na watu binafsi au taasisi yoyote katika kumkomboa
mtoto wa kike” alisema Bi. Khadija Liganga.
Lengo la Mradi wa Binti Box ni kuwapatia elimu ya
uzazi,afya,kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwapatia taulo za usafi
wasichana wa sekondari na shule za msingi waliopo katika umri wa kuvunja
ungo katika mikoa ya Mwanza na Mara. Mradi unatekeleza mpango wa taifa
kwa vitendo wa kuhakikisha watoto wa kike hawabaki nyuma bali wanapata
fursa sawa na wenzao wa kiume na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni