.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 21 Machi 2016

LORI LAPARAMIA MSAFARA WA KAMATI YA BUNGE HUKO BAGAMOYO, WATU WANNE WAFARIKI DUNIA PAPO HAPO

Watu wanne wamefariki dunia na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya kutokea ajali mbaya ya barabarani katika eneo la Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. 

Ajali hiyo imehusisha lori lililoacha uelekeo wake baada ya kupitwa na gari dogo ghafla katika eneo lenye mlima na kwenda kuyagonga magari matatu yaliyokuwa katika msafara wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( Tamisemi ) uliokuwa wilayani humo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Waliofariki dunia wametambuliwa kuwa ni Ludovick Palangyo ambaye alikuwa mchumi, Hilda Msele aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango na Uchumi, Khalid Hassan aliyekuwa dereva wa Mkurugenzi.

Wengine ni Makame Ally aliyekuwa dereva wa gari la Tasaf na Tunsiime Duncun aliyekuwa Mwanasheria wa Wilaya. 

Pia watu wengine 8 walijeruhiwa katika ajali hiyo na wengi wao wamehamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni