.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 21 Machi 2016

MABONDIA KUPIMA UZITO MANGO GARDENI JUMAMOSI KWA AJILI YA KUCHEZA MARCH 27 JUMAPILI YA PASAKA

                                                                                                       Na Mwandishi Wetu

MABONDIA waendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa Pasaka march 27 uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam.

Akizungumzia mpambano huo, mratibu wa pambano hilo Rajabu MAhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote wapo tayari kwa kuwa wapo na afya tele na wanaendelea na mazoezi yao ya mwisho mwisho kila mmoja akijitamba kumsambalatisha mwenzake ,ambapo mabondia mahasimu Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wanakutana kwa mara nyingine kwa ajili ya mpambano wao mwingine baada ya ue wa vmwanzo Miyeyusho kuibuka Mbabe

Mpambano mwingine mkali utakuwa ni kati ya bondia Mada Maugo na Abdallah Pazi ambao wametafutana kwa mda mrefu na sasa watamaliza ubishi siku ya jumapili hii.

Super D aliongeza kwa kusema mabondia wote watapima uzito siku ya jumamosi pale katika ukumbi wa Mango Garden na mpambano utafanyika jumapili ya Pasaka Matrch 27 uwanja wa ndani wa Taifa

'Super D' amesema mbali ya mipambano hiyo inayosubiliwa kwa hamu na mashabiki lukuki, kutakuwa na mipambano ya kukata na shoka mingine ambapo bondia Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha Cosmas Cheka na Mohamed Matumla

Katika mpambano huo kutakuwa na uuzwaji wa vifaa vya mchezo wa ngumi pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa ajili ya kutambua sheria mbalimbali za mchezo zitakazokuwa zikitolewa bure kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa gharama nafuu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni