Timu ya Manchester City imetinga
robo fainali ya Klabu Bingwa Barani Ulaya licha ya kutoa sare tasa
katika mchezo mkali na Dynamo Kiev.
Manchester City, iliyopata faida ya
ushindi wa mechi ya awali wa mabao 3-1, waliumudu vyema mchezo huo
lakini watawakosa mabeki wao Vincent Kompany na Nicolas Otamendi
walioumia.
Beki Vincent Kompany akiwa amekaa chini baada ya kuumia
Katika mchezo mwingine mchezaji
Juanfran afunga penati ya ushindi wakati Atletico Madrid ikiifunga
PSV Eindhoven penati 8-7 katika mchezo wa Klabu Bingwa Barani Ulaya
ulioamuliwa kwa matuta.
Timu hizo mbili zilishindwa
kufungana ndani ya dakika 210 za michezo yao yote miwili, ikiwa ni
mara ya kwanza wa Klabu Bingwa Barani Ulaya kuishia sare ya 0-0
katika michezo yoye miwili.




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni