.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 19 Machi 2016

MASANDUKU YENYE KARATASI ZA KUPIGIA KURA YAWASILI KISIWANI PEMBA

Wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar wakishusha Karatasi za Kupigia Kura baada ya kuwasili Kisiwani Pemba kwa Ndege Maalum ya Kukodi Chini ya Ulinzi Mkali, Kwa ajili ya matumizi ya Uchaguzi kesho, Wananchi wa Zanzibar watashiriki katika Zoezi hilo la Uchaguzi wa Marudio unaotarajiwa kufanyika Zanzibar Nchima kuwachagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani.
Viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe;Mwanajuma Majid Abdall mwenye mtandio Mweusi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba Shekhan Mohamed Sheikhan, maafisa kutoka Tume ya Uchaguzi Pemba na viongozi wa Vyama vya siasa wakishuhudia Uteremshwaji wa karatasi hizo za kupigia kura katika Uwanja wa Ndege kisiwani Pemba
MASANDUKU maalumu yaliyobeba karatasi za kupigia kura zikipakiwa katika magari maalumu ya Jeshi la wananchi wa Tanzania, baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Pemba na kupelekwa katika ofisi ya Tume Chake Chake
MASANDUKU maalumu yaliyobeba karatasi za kupigia kura zikipakiwa katika magari maalumu ya Jeshi la wananchi wa Tanzania, baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Pemba na kupelekwa katika ofisi ya Tume Chake Chake
MAGARI maalumu ya Jeshi la wananchi wa Tanzania, yaliyobeba masanduku yenye karatasi za kupigia kura yakiwa yamewasili kuteremsha karatasi hizo katika ofisi ya Tume ya Uchaguzi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba) Kwa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni