Filimbi zimepulizwa na baadhi ya wabunge kabla ya rais
Uhuru Kenyatta hajasimama kutoa hutuba yake mwaka kwa taifa bungeni.
Spika wa Bunge Justini Mururi alilazimika
kuingilia kati ili kuleta utulivu na kusoma vifungu vya kanuni za
bunge, hata hivyo rais Kenyatta alipoanza kuhutubia filimbi zikaibuka
tena.
Kufuatia filimbi hizo wabunge Opiyo Wandayi, Millie
Odhiambo, Simba Arati, John Mbadi, Gladys Wanga na Seneta Moses
Kajwang waliamuriwa kutoka nje ya bunge.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni