Jumanne, 1 Machi 2016
MKUTANO MKUU WA LAPF KUFANYIKA MACHI 10-11, 2016 UKUMBI WA AICC JIJINI ARUSHA
Na Dotto Mwaibale
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja na bilioni 87 za thamani ya uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.
Hayo yalibainishwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF James Mlowe wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika Machi 10 na 11 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
Alisema LAPF imeendelea kupiga hatua kila mwaka ukilinganisha na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii hapa nchini.
" LAPF imeweza kutoa mikopo ya masomo kwa watu 800 katika maeneo mbalimbali nchini yenye thami ya sh.bilioni 1.2 jambo ambalo tunajivunia" alisema Mlowe.
Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika kwa wadau wa mfuko huo kupatiwa barua za mualiko.
Alisema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene na kuwa mawaziri wengine watakaoshiriki kwenye mkutano huo ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Jafo Selemani .
Alisema katika mkutano huo Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atatoa taarifa ya hesabu za mfuko huo na pia kutakuwa na mada inayohusu afya kutoka kwa Daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
( Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni