.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 24 Machi 2016

MTUHUMIWA WA MASHAMBULIZI YA PARIS KUTOPINGA KUSAFIRISHWA UFARANSA

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya Jijini Paris, Salah Abdeslam, hatopinga kupelekwa Ufaransa akitokea Ubelgiji anaposhikiliwa, wakili wake amesema.

Salah Abdeslam ni miongoni mwa watuhumiwa muhimu wa tukio la mashambulizi ya Paris Novemba mwaka jana yaliyouwa watu 130.

Salah Abdeslam alikamatwa na kujeruhiwa katika msako kwenye nyumba Jijini Brussels siku ya Ijumaa.

Jumanne wiki hii washambuliaji wa kujitoa mhanga walijilipua Jijini Brussels na kuuwa watu 31. Mashambulizi hayo yanadhaniwa kuwa na uhusiano na mtandao wa Abdeslam aliyekamatwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni