.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 19 Machi 2016

MTUHUMIWA WA SHAMBULIZI LA PARIS AKAMATWA JIJINI BRUSSELS

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya Paris Salah Abdeslam amejeruhiwa na kukamatwa katika msako uliofanyika Jijini Brussels baada ya kutafutwa kwa kipindi cha miezi minne.

Mwanaume mwingine Monir Ahmed Alaaj, pia naye yupo katika orodha ya watu wanaotafutwa na vyombo vya dola mwendesha mashtaka wa Ubegiji amesema.

Wanafamilia watatu wanaotuhumiwa kumpa hifadhi nyumbani kwao mtuhumiwa Abdeslam pia nao wanashikiliwa na polisi.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema anatarajia mtuhumiwa Abdeslam kusafirishwa kwenda Ufaransa haraka iwezekanavyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni