Muuaji wa watu wengi Anders Behring
Breivik amepiga saluti iliyokua ikitumiwa na Nazi wakati alipokuwa
akiingizwa mahakamani kuwasilisha kesi yake ya kulalamikia hali ya
chumba cha gereza alilofungwa huko Norway.
Breivik, 37, aliyewauwa wau 77 mwaka
2011, hakusema neno lolote alipokuwa akiingia mahakamani, na
kuonekana mara ya kwanza kwa umma tangu atiwe hatiani kwa mauaji hayo
yaliyoshitua dunia.
Katika kesi yake hiyo Breivik,
amedai amekuwa akitendewa mambo yasiyoyakibinadamu katika gereza la
Skien lililopo umbali wa mile 87 kusini magharibi mwa Oslo, ambapo
ametengwa kwenye chumba cha peke yake akiwa na komputa na kifaa cha
mchezo PlayStation.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni