.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 8 Machi 2016

MZAHA WAMPONZA MWANAFUNZI WA MISRI ANAYESOMEA URUBANI MAREKANI

Mwanafunzi wa kozi ya urubani wa Misri amekubalia kuondoka nchini Marekani baada ya kuposti kwenye Facebook maneno ya mzaha yasemayo 'dunia itanishukuru iwapo nitamua Donald Trump'.

Mwanafunzi huyo Emadeldin Elsayed, 23, hakufunguliwa mashtaka ila mamlaka za Marekani ziliamua arejeshwe kwao, wakili wake Hani Bushra ameeleza.

Mamlaka ya Idara ya Uhamiaji imesema itamruhusu mwanafunzi huyo kurejea kwao Misri kwa hiyari, iwapo ataondoka mwenyewe hadi ifikapo Julai 5, mwaka huu. Viza ya Elsayed imefutwa na anashikiliwa gerezani California.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni