Mchezaji Aleksandar Mitrovic ameipatia pointi moja muhimu
Newcastle dhidi ya wapinzani wao waliopamoja mkiani timu ya
Sunderland katika pambano kali la kujaribu kukwepa kushuka daraja
lililoishia kwa sare ya 1-1.
Mshambuliaji huyo raia wa Serbia aliunganisha kwa kichwa krosi
ya Georginio Wijnaldum dakika saba kabla ya mpira kuisha na kumpatia
sare ya kwanza kocha mpya wa Newcastle Rafael Benitez. Jermain Defoe
alifunga bao la kwanza kwa Sunderland.
Aleksandar Mitrovic akiupiga mpira kichwa na kujaa wavuni
Jermain Defoe akipiga shuti mpira uliojaa wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni