.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 1 Machi 2016

NGUMI KUPIGWA BAGAMOYO MARCH 5 UKUMBI WA TASUBA

                                                                                   Na Mwandishi Wetu

BONDIA Seba Temba wa kg 66 kutoka mkoa wa Morogoro anatarajia kupanda ulingoni march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo kupambana na mkali wa mkoa huo wa Pwani Iddi Pialali mpambano uho ambao umeandaliwa na Muhsin Sharif.

Promota huyo alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine mengi ya mchezo wa ngumi likiwemo la wanawake Joyce Awino kg 64 na Mariam Tembo na Abdallah Pazi kg 76 atakumbana na Georger Dimoso na Flank Lampad kg 69 atavaana na Mwaite Juma wakati bondia kutoka mkoa wa Tanga Jacobo Mganga kg 72 atapambana na Maono Ally.

Mpambano huo ni rasmi kabisa kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakazi wa Bagamoyo mkoa wa Pwani pamoja na vitongoji vyake ambao walikuwa wakisubiri burudani hiyo ya mchezo wa masumbwi nchini.

Nae bondia Seba Temba amejinasibu kwa kujigamba lazima amlaze Iddi Pialali na ndio itakayokuwa njia yake ya mazoezi kabla ya kupambana na bondia Pius Kazaula mpambano utakaofanyika march 27 katika uwanja wa ndani wa taifa siku ya sikukuu ya Pasaka.

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile, Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.

Pia kutakuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa ngumi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni