Rais wa Niger, Mahamadou Issoufou,
amechaguliwa tena kwa muhula wa pili kwa kupata ushindi wa kishindo
kwenye uchaguzi wa marudio uliogubikwa na utata.
Tume ya Uchaguzi imesema rais
Issoufou amepata zaidi ya asilimia 90 ya kura zote katika uchaguzi wa
jumapili, ambao wapinzani waliususia.
Mpinzani wake Mkuu, Hama Amadou,
ambaye wiki iliyopita alisafirishwa kwa ndege kwenda Ufaransa kwa
matatibabu amepata kura asilimia 8.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni