.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 7 Machi 2016

SPIKA AFUNGUA MKUTANO KATI YA BAADHI YA WABUNGE NA WADAU WA AFYA

NDG1
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya Bw.Svend Robinson. Walikuwa wakizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano uliowahusisha baadhi ya Wabunge na wadau wa Afya. Mkutano huo ulilenga kujadili kuhusu uwekezaji katika Sekta ya Afya na ulifayika leo tarehe 3 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.
NDG4
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na baadhi ya Wabunge waliohudhuria mkutano wa pamoja na wadau wa Afya kujadaili kuhusu uwekezaji katika sekta ya Afya jijini Dar es Salaam.
NDG5
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa pili kushoto), Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamis Kigwangala pamoja na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya Bw.Svend Robinson wakifuatilia mazungumzo juu ya uwekezaji katika sekta ya Afya. Anayezungumza ni Mwakilishi wa Shirika la Afya hapa nchi Dkt Rufaro Chatora.
NDG6
Baadhi ya Wabunge na Wadau wa Afya wakifuatilia mazungumzo juu ya uwekezaji katika sekta ya Afya hapa nchini.
NDG7
Baadhi ya Wabunge na Wadau wa Afya wakifuatilia mazungumzo juu ya uwekezaji katika sekta ya Afya hapa nchini.
NDG8
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akihutubia wadau mbalimbali wa Afya waliokutana kujadili juu ya uwekezaji katika Sekta ya Afya hapa nchini.
NDG9
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kushoto) Mwakilishi wa Shirika la Afya hapa nchi Dkt Rufaro Chatora (katikakati) na na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya Bw.Svend Robinson wakijadili jambo mara baada ya ufunguzi wa Mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Afya kujadili juu ya uwekezaji katika Sekta ya Afya hapa nchini.

                                                                                             (Picha na Ofisi ya Bunge)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni