.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 7 Machi 2016

WAZAZI WAOMBA SEREKALI KUCHUNGUZA KWANINI WATOTO WAO WANAFELI SANA WILAYANI KARATU

                                                                                          Na Woinde Shizza,Karatu

Wazazi wa vijiji vya Kata ya Barai iliyoko Wilayani Karatu Mkoani
Arusha wameiomba serikali ya awamu yaa tano kuchunguza sababu za
watoto wao kufanya vibaya katika mitahani ya kuhitimu darasa la saba.

Wazazi hao wametoa kilio hicho kufuatia ufauulu duni wa mara kwa mara
kwa watoto wanaohitimu darasa la saba ambapo wanafunzi hao wamekuwa
wanahitimu wakiwa hawajui kusoma wala kuandika na kushika nafasi za
mwisho kitaifa katika mtihani wa darasa la saba jambo ambaalo  wanaliona kama kuwapotezea muda watoto hao ambapo wazazi hao wakiwa  wanawaitaji kuwachungisha mifugo.

Aidha Kata hii ya Barai yenye shule 12 za msingi ambapo kati ya shule  hizo shule sita zimefanya vibaya kitaifa na zimeshikilia nafasi za  mwisho kabisa kitaifa ambapo alisema shule sita izo zipo katika nafasi  za shule kumi zilizofanya vibaya kitaifa katika mtiani wa darasa la saba kwa mwaka jana.

Mwandishi wa habari hizi alitembelea shule tatu za Kata hiyo kujua  sababu zinazosababisha kutafaulu kabisa kwa wanafunzi ambapo taarifa  zinaonyesha kuwa shuke hizo zina walimu sita pekee ikiwa na  maana kila shule yenye madarasa saba ina walimu wawili
 

Wakizungumzia sababu za shule hizo kufanya vibaya mmoja wa mwalimu wa
shule ya msingi Gidamilanda Paul Hando alisema kuwa ni pamoja na
umbali mrefu ambao wanafunzi wanalazimika kutembea wakija mashuleni ambapo wanatembea zaidi ya kilimeta 24 kwenda shuleni ,pamoja na
wanafunzi kutumia muda mwingi kuchunga mifugo badala ya kujisomea
pindi wanapotoka mashuleni.

Aidha alibainisha kuwa mbali na tatizo la umbali mrefu pia wanafunzi
wamkuwa wakisumbuliwa na tatizo la njaa kwani shule hizo zimekuwa
hasipikii wanafunzi mashuleni mchana kutokana na kutokuwa na bajeti
hiyo .



Kwa upande wake mmoja wanafunzi hao ambao alijitambulisha kwa jina la
Gilony Gitonyi alisema kuwa wamekuwa wanashindwa kusoma kutokana na
njaa pamoja na kukosa mda wa kujisomea pindi wanaporudi nyumbani kwani
muda mwingi wamekuwa wakiutumia kwa ajili kuchunga mifugo pindi
wanaporudi majumbani.

Akizungumzia swala hilo mbunge wa jimbo la karatu Willy Qambalo
alisema kuwa kwa upande wake anaona suluhisho la kutatua tatizo hilo
ni pamoja na kujenga mabweni ilikuweza kuwasadia wanafunzi kupata
elimu ili kila mwanafunzi asome apoapo shuleni ili kuweza kujipatia
muda wa kujisomea.

"unajua kujengwa kwa haya mabweni pia itasiadia kuwapata wanafunzi
kirahisi ambao muda wamekuwa wakiacha masomo na kwenda kuchunga
mifugo jambo ambalo linapingwa vikali na wazazi wa vijiji hivyo na pia
wanafunzi hao watapata muda mrefu wa kujisomea na swala wao kupata
njaa litapungua kwani kutakuwa na chakula shuleni kwa ajili  yao"alisema Qakambalo
 

Aidha Tafiti zinaonyesha walimu ,wenye utovu wa nidhamu watoro na  walevi katika maeneo ya mijini ndio hupelekwa katika shule hizzo  zilizoko maeneo ya porini kama adhabu kwao.Swali la kujiuliza je  mwalimu huyu atakuwa na nia ya kuwafundisha wanafunzi?Kupelekwa kwa  mwalimu huyu kama adhabu badala ya eyey kuridhia Kujua kusomaa na  kandika kwa wanafunzi hawa itakuwa ni ndoto

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni