.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 31 Machi 2016

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA INTANETI, AfPIF 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba akielezea matumizi ya intaneti yalivyo nchini na changamoto zinazowakabili watumiaji wa huduma hiyo. (Picha na Modewjiblog)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary.
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto), Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary, Meneja Mradi wa Tanzania Internet Exchange (TIX), Frank Habicht na Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi wakizungumza jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo
Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary akifungua mkutano huo.

Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi akizungumzia mkutano wa Intaneti, AfPIF utakaofanyika nchini, Agosti, 30 - Septemba, 1
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo.
Baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano huo.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

Mwaka 2016 unakuwa mwaka wa neema kwa Tanzania kupata fursa ya kuandaa Mkutano unaowakutanisha wadau wa intaneti (African Peering and Interconnection Forum), mkutano unaotaraji kufanyika Agosti 31 – Septemba 1, jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mkutano huo, Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi amesema mkutano huo unalengo wa kukutanisha wadau mbalimbali wa intaneti ili kutanua miondombinu ya intaneti katika bara la Afrika.

Amesema taasisi yake inapenda kuona huduma ya intaneti ikipatikana kwa urahisi kwa watumiaji wake Afrika na hivyo kupitia mkutano huo wataweza kutazama jinsi gani wanaweza kushirikiana na kubadilishana takwimu za watumiaji wa mitandao kwa bara zima la Afrika.

“Tunatambua kuwa watumiaji wa intaneti wanazidi kuongezeka na kupitia mkutano huu tutaweza kuangalia jinsi gani tunaboresha huduma ya intaneti iwe bora ili iweze kutumiwa na watu wengi zaidi,” amesema Mwangi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba amesema mkutano huo una umuhimu kwa Watanzania kwa kupata fursa ya kujifunza na kubadilishana mawazo na watu kutoka mataifa mengine katika huduma ya intaneti.

Amesema kwa sasa Tanzania bado ina changamoto nyingi katika huduma ya intaneti na kupata nafasi hiyo ya kuandaa mkutano kutakuwa na faida kwa mashirika yanayotoa huduma ya intaneti ili kuwawezesha kutambua ni jinsi gani wataboresha huduma kwa wateja.

“Nchi yetu inawatumiaji wengi wa intaneti ila bado kuna changamoto nyingi ikiwepo usalama wa mtandao na serikali inafanya jitihada nyingi kumaliza changamoto hizo na kupitia mkutano huu tunaamini utasaidia zaidi Watanzania kupata kitu kipya katika huduma ya intaneti,” amesema Simba.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary amesema Watanzania wengi bado hawajafahamu umuhimu wa intaneti kutokana na kutokuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu intaneti lakini kupitia mkutano huo ulioandaliwa na Internet Society wataweza kuapata elimu mpya kuhusu intaneti.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni