.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 19 Machi 2016

TIMU YA LEICESTER CITY HAIKAMATIKI LIGI KUU YA UINGEREZA

Timu ya Leicester City imejikita kileleni zaidi kwa tofauti ya pointi nane kufuatia goli la Riyad Mahrez kutosha kuilaza Crystal Palace ambao walionekana kuiwekea ngumu mno klabu hiyo.

Riyad Mahrez alipoteza nafasi nzuri ya kwanza ya wazi, lakini alirekebisha makosa baadaye na kupachika bao akiunganisha krosi ya Jamie Vardy.
Kwa upande wake timu ya Arsenal imerejea kwa kishindo baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Barani Ulaya na FA kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 katika dimba la Goodison Prak.

Danny Welbeck alikuwa wa kwanza kufunga bao katika dakika ya saba, na baadaye katika dakika ya 42 kinda Alex Iwobi alifunga goli na kuweka rekodi ya kufunga goli lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza.
                                         Danny Welbeck akifunga bao la kwanza kwa Arsenal 
Katika mchezo mwingine Cesc Fabregas alifunga magoli mara mbili likiwemo la penati ya dakika za mwisho na kuisaidia Chelsea kutoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya West Ham.

West Ham ilikuwa yakwanza kuongoza baada ya Manuel lanzini kumpa wakati mgumu kipa Thibaut Courtois kushindwa kuudaka mpira wa kuzungusha wa shuti la umbali wa yadi 25.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni