.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 27 Machi 2016

UINGEREZA YAIDUWAZA UJERUMANI KWA KIPIGO WAKIWA NYUMBANI KWAO

Timu ya Taifa ya Uingereza imetoka nyuma na kuweza kuwafunga mabingwa wa Kombe la Dunia Ujerumani kwa maboa 3-2, huku kizazi kipya cha Uingereza katika soka kikifanya vizuri katika mchezo huo uliopigwa Jijini Berlin.

Katika mchezo huo Ujerumani ilionekana kama itaharibu mipango ya Uingereza kung'ara kwa magoli yaliyofungwa na Toni Kroos la shuti la masafa na kumshinda kipa Jack Butland, na baadae Mario Gomez kufunga la pili kwa kichwa.

Dele Alli alicheza vyema na kumuunganishia Harry Kane aliyepachika bao na Jamie Vardy akafunga goli lake la kwanza katika mchezo wa kimataifa kutokana na krosi ya Nathaniel Clyne na Eric Dier akapachika la tatu kwa kichwa.
                   Mpira uliopigwa na Gomez ukimpita kipa wa Uingereza Jack Butland
                             Jamie Vardy akituliza mpira kati kati ya mabeki wa Ujerumani

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni