

Mtoa Mada, Suzane Ngane kutoka Cameroun, akitoa mada kwenye mkutano huo.








Baadhi yawashiriki wakifuatilia kwa makini yanayoendelea katika mkutano


Na Beda msimbe
Wataalamu
wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali duniani
wameanza mkutano wa siku mbili jijini Dare s Salaam kuangalia namna ya
kuwezesha fedha za kusaidia maendeleo endelevu kwa kutumia vyanzo vya
ndani.
Mkutano
huo wa siku mbili ulioanza jana katika hoteli ya Hyatt Regency,
Kilimanjaro umelenga kuja na maelezo muafaka ya namna ya kupata fedha za
kuendesha na kujenga miundombinu mbalimbali kwa ajili ya miji
inayotanuka.
Katika
mahojiano na mwandishi wa Mo Blog kuhusu mkutano huo , mmoja wa
wakurugenzi wa UNCDF kutoka makao makuu anayeshughulikia uendelezi wa
fedha, David Jackson alisema kwamba wataalamu walioalikwa wanatarajiwa
kutoka na msimamo unahusu uwezeshaji wa fedha wa ndani.
Alisema
wakati dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ya wananchi kutoka
vijijini kwenda mijini uwezo wa majiji mengi duniani ikiwamo manispaa ni
mdogo kuwezesha kutengeneza miundombinu na pia kuwezesha ajira.
Alisema
kwa sasa kutokana na uwingi wa watu wanaofurika katika miji,
halmashauri na uhaba wa fedha kutoka katika vyanzo vya mapato
kumesababisha kushindwa kuendelezwa mifumo endelevu ya miundombinu na
ajira na kulazimisha wataalamu kuanza kuangalia namna nyingine ya kupata
fedha.
Alisema
mpango wa kutafuta vyanzo vingine vya fedha kwa kuunganisha nguvu nje
ya mfumo rasmi umewezekana Tanzania hasa kutokana na manispaa kama ya
Kibaha kuwezeshwa kupata fedha za miradi mbalimbali na wengine nao
watatoa uzoefu wao.
“Zamani
ilikuwa rahisi sana kwa manispaa nyingi kutengeneza mipango ya
maendeleo, lakini kwa sasa kutokana na uwingi wahamaji vyanzo vya
kawaida vimezidiwa na kuonekana haja ya kutafuta vyanzo vingine ili
kuwezesha maendeleo na ajira,” alisema Jackson.
Alisema
mataifa yanahitaji sasa kuangalia mifumo yao ya kuwezesha maendeleo
endelevu kwa kutumia vyanzo vya ndani ambavyo vinawezekana kupatikana.
Aliongeza
kuwa miradi mikubwa ya maendeleo haiwezi kufanywa na vyanzo vya zamani
na kutolea mfano mradi wa maji wa Abu Dhabi ambao umewezeshwa kwa
kutumia vyanzo vya ndani lakini kwa namna ambayo inasaidia mji huo kuwa
na maji ya uhakika pamoja na kwamba vyanzo vyake havifai.
Alisema
ni matumaini yake kwamba baada ya kusikiliza mada mbalimbali wataalamu
hao watakuwa na nafasi ya kutoa tamko la namna bora ya kushirikisha
wadau wa maendeleo wa ndani kutengeneza miradi mikubwa ya huduma kwa
jamii.
Pia
alisema kwamba washiriki katika mkutano huo wa siku 2 ni pamoja na
wadau wa maendeleo kutoka Uswisi, Sweden na Denmark wapo pia wataalamu
wa masuala ya fedha, miradi kutoka Afrika Kusini, Ethiopia, Benin,
Rwanda, Mali, Senegal,Uganda, Msumbiji, india, Bangladesh , Marekani na
Tanzania.
Mkutano
huo wa mashauriano uliandaliwa na UNCDF ikiwa ni sehemu ya utekelezaji
wa azimio la AddisAbaba kuhusu maendeleo endelevu na umuhimu wa
kuimarisha uwezo wa kifedha wa manispaa mbalimbali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni