Matumaini ya Chelsea kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa
Ulaya yamemalizwa baada ya kutolewa katika raundi ya 16 bora na Paris
St-Germain kwa kuchapwa mabao 2-1 katika dimba la Stamford Bridge.
Ushindi huo wa PSG umechochewa na jitihada za Zlatan
Ibrahimovic ambaye alipiga mpira wa krosi uliomaliziwa vyema na
Adrien Rabiot na kuandika bao la kwanza hata hivyo Diego Costa
alisawazisha baadae.
Katika mchezo huo Costa alitolewa nje baada ya kuumia na
kuiacha Chelsea ikijikuta ikipachikwa bao la pili na Ibrahimovic
aliyemalizia kiulaini pande la Angel di Maria na kuipeleka PSG katika
hatua ya nane bora.
Zlatan Ibrahimovic akipachika bao la pili kwa PSG
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni