Magoli matatu ya Andy Caroll kwa lugha ya soka
hat-trick yameleta pigo kwa timu ya Arsenal ambayo tayari inanafasi
finyu ya matumaini ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza licha ya
washika mtutu hao kulazimisha sare ya mabao 3-3 dhidi ya West Ham.
Arsenal ambayo ipo pointi 10 nyuma ya vinara wa
Leicester City ikiwa na michezo sita iliyobakia, ilipata bao la
kwanza kupitia kwa Mesut Ozil na Alexis Sanchez kuongeza la pili
baada ya kupatiwa pande na Alex Iwobi na kuongoza kwa mabao 2-0.
Hata hivyo Andy Caroll alipachika mabao mara mbili
ndani ya sekunde 160, na kuifanya West Ham kusawazisha, na kisha
baadaye katika kipindi cha pili alipiga kichwa kilichoingia kwenye
posti na kuandika bao la tatu kabla ya Laurent Koscielny kuisawazisha
Arsenal.
Andy Caroll akiwa kazini, hakika leo alikuwa mwiba mkali dhidi ya Arsenal
Alexis Sanchez akimshukuru alex Iwobi kwa kumpa pande lililozaa bao la pili kwa Arsenal
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni