.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 9 Aprili 2016

KIPIGO CHAISUKUMA NEWCASTLE KUELEKEA KATIKA KUNDI LA KUSHUKA DARAJA

Timu ya Newcastle imeendelea kuporomoka karibu na kundi la kushuka daraja baada ya kushindwa kiulaini na Southampton kwa kukubali kipigo cha mabao 3-1 katika dimba la St Mary.

Alikuwa Shane Long aliyeipatia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya nne na kisha Graziano Pelle aliongeza la pili katika mchezo ambao Southampton walianza vizuri wakiwa katika dimba la nyumbani.

Southampton waliandika bao la tatu katika kipindi cha pili kupitia kwa Victor Wanyama aliyeachia shuti kali la karibu, huku Newcastle wakipata bao pekee la kufutia machungu ya kipigo hicho kupitia kwa Andros Townsend.
                                                        Victor Wanyama akishangilia goli lake
            Graziano Pelle akijipinda kuachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni