Askofu Mkuu wa Canterbury amesema matokeo ya
vipimo vya DNA vilivyosaidia kubaini baba yake halisi vimemshangaza.
Askofu huyo Justin Welby, 60, wa Kanisa la
Anglikana amebaini kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Katibu wa Sir Winston
Churchill aitwae Sir Anthony Montague Browne.
Awali Askofu Welby alikuwa anaamini kuwa ni mtoto
wa muuza mvinyo Gavin Welby, ambaye alifariki dunia mwaka 1977.
Mama wa Askofu Welby, Lady Williams wa Elvel,
amethibitisha kuwa alikuwa na mahusiano na Sir Anthony, kabla ya
kuolewa mwaka 1955.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni