Baba Askofu Samuel Yesaya Mwaiseje wa Kanisa la Moravian Jimbo la Mashariki linalohudumia ukanda wa Pwani, Morogoro, Lindi, Zanzibar na Mtwara akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ASli Iddi aliyefiki Ofisini kwake Vuga kumpongeza kwa kuteuliwa kushika tena wadhifa huo.
Mchungaji wa Kanisa la Moravian Jimbo la Mashariki kwa hapa Zanzibar Rev osiah Radoni Siwelwe mwenye suti ya buluu akimueleza Balozi Seif mikakati yao katika kuimarisha huduma za Kijamii kama Afya na Elimu hapa Zanzibar.
Kushoto mwa mchungaji Siwelwe ni Baba Askofu Samuel Yesaya Mwaiseje wa Kanisa la Moravian Jimbo la Mashariki.
Kushoto mwa mchungaji Siwelwe ni Baba Askofu Samuel Yesaya Mwaiseje wa Kanisa la Moravian Jimbo la Mashariki.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Uongozi wa Kanisa la Moravian Jimbo la Mashariki linalohudumia ukanda wa Pwani, Morogoro, Lindi, Zanzibar na Mtwara umehidi kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhudumia Wananchi katika sekta za Afya na Elimu.
Baba Askofu Samuel Yesaya Mwaiseje wa Kanisa hilo alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza kwa Kuchaguliwa kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda pamoja na kuteuliwa tena na Rais wa Zanzibar Kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Baba Askofu Samuel Yesaya Mwaiseje akiwa na mchungaji wa Kanisa hilo hapa Zanzibar Rev Osiah Radoni Siwelwe alisema lengo la uongozi wa Kanisa hilo katika kuelekeza nguvu zao katika miradi ya kijamii ni kuweka uhusiano wa karibu zaidi na Serikali.
Alisema huduma za ibada sambamba na zile za Kijamii za Kanisa hilo tayari zimeanza kutolewa katika Kisiwa cha Unguja tokea mwaka 2008 ambapo kwa sasa wanaendesha na kusimamia skuli inayotoa taaluma kwa watoto wowote wa Visiwa hivi bila ya kujali imani zao za kidini.

Baba Askofu Mwaiseje alifahamisha kwamba malengo ya baadaye ya Uongozi wa Kanisa hilo la Moravian ni kuanzisha vituo vya kulelea Watoto, kurekebisha Vijana waliathirika na Dawa za kulevya pamoja na matunzo ya watu walioathirika na Ukimwi.
“ Kanisa letu mbali ya kuendelea kutoa huduma za Afya na Elimu lakini pia tumejipanga kuanzisha vituo vya kulelea watoto, Dawa za Kulevya na Ukimwi ”. Alisema Baba Askofu Samuel Yesaya Maiseje.
Akitoa shukrani zake kwa Uongozi huo wa Jimbo la Mashariki wa kanisa la Moravian Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa kila msaada katika kuona Taasisi za Kidini zinafanikiwa vyema katika malengo yao ya kutoa huduma za Kijamii.
Balozi Seif alionya kwamba Serikali haitakuwa tayari kuona baadhi ya watu wanajitokeza kuanzisha tabia za kufanya ubabe katika kuwabughudhi waumini wa Taasisi hizo katika kuimarisha malengo yao.
Alisema Katiba ya Nch iko wazi bila ya ubaguzi ikitoa mamlaka na fursa kwa kila wananchi kuwa na uhuru wa kufuata dini anayoiamini katika nafsi yake.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
15/4/2016.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni