.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 14 Aprili 2016

BARCELONA NJE, YAVULIWA UBINGWA WA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wametolewa katika michuano hiyo wakati magoli mawili ya Antoine Griezmann yakiibeba Atletico Madrid na kutinga katika nusu fainali za michuano hiyo.

Barcelona iliwasili katika Jiji la Madrid ikiwa na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa awali lakini uzembe wa mabeki wake ulimfanya Griezmann ambaye alikuwa hana mtu wa kumkaba kupachika bao la kwanza na kisha baadaye kupachika la pili kwa penati.
                                                                   Antoine Griezmann akipachika bao 
                    Wachezaji wa Barcelona wakimlalamikia refa kwa maamuzi yake
Katika mchezo mwingine Bayern Munich ilifanikiwa kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kupambana na kiume na Benfica na kutoka sare ya mabao 2-2.

Timu hiyo ya Ureno iliyokuwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa awali, walijipa matumaini baada ya Raul Jimenez kupachika bao la kwanza katika mchezo wa jana.

Hata hivyo Arturo Vidal na Thomas Muller walifunga magoli na kuiweka klabu hiyo ya Ujerumani katika nafasi ya kusonga mbele licha ya Talisca kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 2-2.
                                                                        Arturo Vidal akitikisa nyavu

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni