Nchi ya China imebainisha mkakati wa kuwa taifa
kubwa katika soko duniani ifikapo 2050, ikiwa na mipango ya kuwapata
watoto milioni 50 na watu wazima wanaocheza soka ifikapo 2020.
Malengo mengine ni pamoja na kuwa na vituo vya
mafunzo vipatavyo 20,000 pamoja na viwanja 70,000 ifikapo 2020.
Hayo yanakuja wakati China ikitakata kwenye
michezo ya Olimpiki na Olimpiki Maalum na iliwahi kufuzu katika kombe
la dunia mwaka 2002.
Rais Xi Jinping ni mpenzi wa mpira wa miguu na
awali aliwahi kusema anataka kuona China inatwaa Kombe la Dunia
katika kipindi cha miaka 15.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni