.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 8 Aprili 2016

DUA YA KUMUOMBEA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR MZEE KARUME

Mjukuu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Ahmed Amani Abeid Karume akichukua shada la mauwa kwaniaba ya wenzake kuliweka katika kaburi baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea Marehemu Babu yao, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli,(wa pili kulia) pamoja na Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa,[Picha na Ikulu.]
Wake wa Viongozi wakiwa nje ya Ofisi Kuu wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar baada ya kumalizika kwa hitma ya kumuombea dua Rais wa kwaanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeeid Amani Karume iliyofanyika leo,[Picha na Ikulu.]
Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa,[Picha na Ikulu.]
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanawema Shein (kushoto) Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume,Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi pamoja wake wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akifuatana na wasaidizi wake akitoka eneo la kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume liliopo nje ya Jengo la Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar baada ya kumalizika hafla ya dua na uwekaji wa mashada ya mauwa iliyofanyika leo,na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono viongozi na wananchi walihudhuria katika hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo baada ya kumalizika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar na uwekaji wa mashada ya mauwa ambapo Viongozi na Wananchi mbali mbali walihudhuria,[Picha na Ikulu.]

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni