Kongozi wa mapinduzi ya Cuba Fidel
Castro, 89, ametoa hutuba iliyoibua hisia kali katika mkutano wa
chama cha Kikomonisti iliyoashiria kuwa muda wake wa kuishi duniani
unaisha.
Katika mkutano huo Castro amesema
hivi karibuni atafikisha miaka 90, na kama ilivyo kwa binadamu
wengine maisha yake yatafikia ukomo.
Amesema kuwa kisiwa hicho
kitaendelea kutawaliwa na wananchi wa Cuba wenyewe hata kama viongozi
wake wa mapinduzi wamezeeka na kufariki dunia.
Fidel Castro akihutubia mkutano wa chama cha Kikomonisti
Rais Raul Castro (mwenye suti) ambaye ni mdogo wa Fidel Castro akipiga makofi baada ya Fidel kumaliza hotuba yake



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni