.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 21 Aprili 2016

LIVERPOOL, MANCHESTER UNITED ZAUA KATIKA LIGI KUU YA UINGEREZA

Kikosi cha Kocha Jurgen Klopp kimepata ushindi mzuri baada ya Liverpool kuifunga Everton iliyokuwa na wachezaji 10 kwa mabao 4-0 ikiwa ni ushindi wao wa tatu mfululizo katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Walikuwa wachezaji Divock Origi na Mamadou Sakho waliofunga kwa kichwa mabao mawili katika kipindi cha kwanza, kabla ya Daniel Sturridge na Coutinho kufunga mengine mawili katika kipindi cha pili.
                Divock Origi akiruka juu na kupiga mpira kwa kichwa uliojaa wavuni
Nayo Manchester United ipo nyuma kwa pointi moja dhidi ya Arsenal iliyokuwa katika nafasi ya nne ya ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace.

Katika mchezo huo Manchester United ilizawadiwa goli la kwanza baada ya Damien Delaney kujifunga kwa kuunganisha mpira wa krossi uliopigwa na Matteo Darmian, ambapo baadaye tena Darmian aliongeza goli la pili kwa shui la yadi 20. West Ham 3-1 Watford.
                      Damien Delaney akijifunga goli na kumpoteza mahesabu kipa wao
                                  Kipa wa Crystal Palace akipangua shuti la Anthony Martial

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni