.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 21 Aprili 2016

MKUU WA WILAYA IRINGA MH. RICHARD KASESELA AONGOZA MAPOKEZI YA MWILI WA BRIG' JENERALI MSTAAFU ERNEST GALINOMA

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela ( kushoto ) akiwa na makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) katika mapokezi ya mwili wa Brig General (Mstaafu) Ernest Galinoma nyumbani kwake Kalenga. 

Jana tarehe 20/04/2016 usiku Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela aliongoza waombolezi katika mapokezi ya mwili wa Brig General (Mstaafu) Ernest Galinoma nyumbani kwake Kalenga. 

Marehemu alifariki juzi jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kalenga.

Shughuli za ibada zitaanza saa 6 mchana katika kanisa katoliki Kalenga. Bwana ametoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) wakiteremsha mwili wa Brig General (Mstaafu) Ernest Galinoma baada ya kuwasili nyumbani kwake Kalenga.
Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) wakiwa wamebeba jeneza lenye  mwili wa Brig General (Mstaafu) Ernest Galinoma kuuingiza nyumbani kwake Kalenga.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni