.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 15 Aprili 2016

LIVERPOOL YAPAMBANA KIUME NA KUTINGA NUSU FAINALI LIGI YA UROPA

Timu ya Liverpool imepambana kiume ikitokea nyuma baada ya kufungwa na kutinga nusu fainali za Ligi ya Uropa kwa kuifunga Borussia Dortmund mabao 4-3 katika dimba la Anfield.

Katika mchezo huo Henrikh Mkhitaryan aliipatia Borussia Dortmund bao la kwa kwa shuti kali la karibu katika dakika ya tano, kabla ya Pierre Emerick-Aubameyang kuongeza la pili kwa kumalizia vizuri mpira katika eneo la penati.

Hata hivyo mwisho wa siku Dejan Lovren, Mamadou Sakho, Phillipe Coutinho pamoja na Divock Origi waliokoa jahazi la kocha Jurgen Klopp lisizame baada ya kupachika magoli na kufanya matokeo ya ujumla na mchezo wa mwanzo kuwa mabao 5-4.
Dejan Lovren akiruga juu angani na kupiga kichwa kiliozaa bao la nne la Liverpool katika ya dakika ya 90.
                    Pierre Emerick-Aubameyang akiruka sarakasi kushangilia goli lake
          Wachezaji wa Liverpool Origi na Sakho wakipiga selfie baada ya ushindi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni