.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 1 Aprili 2016

MAZISHI YA MNYARWANDA ALIYE FARIKI KWENYE AJALI IRINGA YAMEFANYIKA JANA MAKABURI YA MKANYAGENI

Jana 31/03/2016, Mkuu wa wilaya Iringa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa ameshiriki kwenye mazishi ya Mnywarwanda Jeannnete Mukashema aliyefariki kwenye ajali iliyotokea usiku Juzi. Bi Jeanette alikuwa akisafiri na mtoto wake ( pichani juu akiwa na mkuu wa wilaya ) ambaye naye aliumia kwenye ajali hiyo na bado anaendelea na matibabu.
Akizungumza katika mazishi hayo, Mh Kasesela alisema, " Imeniuma sana kwani niliupokea mwili kwa mikono yangu tukiwa na waokoaji wengine alipo tolewa juu kwenye basi, ni wazi bado tukio hilo limo mawazoni mwangu na nguo zangu zikiwa na madoa ya damu , tulimpokea akiwa tayari amefariki.
Mkuu huyo wa wilaya ya Iringa aliendelea kusema kuwa, " Kesho yake mtoto alipozinduka akaanza kumtafuta mama yake, nilipomtembelea asubuhi, nilijua mama yake amefariki dunia nilishindwa kumwambia leo alipo niona ameanza kulia amenikumbusha nikiwa miaka 11 nilipo ondokewa na mama yangu. lakini naamini yuko katika mikono salama, Mungu ni mwema baba yake na ndugu wengine wamekuja kutoka Rwanda, alisema Kasesela.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni