Utafiti mkubwa uliofanywa
umebainisha kuwa dunia kwa sasa inawatu wazima zaidi waliofikia
kigezo hatari cha kiafya cha unene wa kupindukia, kuliko walio na
uzito mdogo.
Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa
Chuo cha Imperial cha London na kuchapishwa kwenye jarida la
madaktari la The Lancet, imelinganisha uzito wa mwili wa watuwazima
milioni 20 wanaume na wanawake tangu mwaka 1975 hadi 2014.
Utafiti huo umebaini unene
uliopindukia kwa wanaume umeongezeka mara tatu, ikilinganishwa na
wanawake ambao wao umeongezeka maradufu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni