Mhamiaji raia wa Irani mwenye miaka
23, aliyejichoma moto akiwa kwenye kituo cha kuwashikilia wakimbizi
nchini Australia katika kisiwa cha Nauru amefariki dunia.
Idara ya Uhamiaji ya Australia
imethibitisha mhamiaji huyo mwanaume huyo amefariki dunia akiwa
kwenye hospitali Brisbane hii leo.
Mhamiaji huyo aliyejulikana kwa jina
la Omid, alijichoma moto katika kituo hicho cha kuwashikilia
wakimbizi siku ya jumanne, na kuungua vibaya sehemu kubwa ya mwili.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni