Matumaini ya timu ya Liverpool
kutinga fainali za Ligi ya Uropa kwa mara ya kwanza tangu kupita
karibu muongo moja yamepata pigo baada ya Villarreal kuifunga goli
moja katika dakika za majeruhi katika mchezo wao wa kwanza.
Katika mchezo huo Liverpool
ilikaribia kupata goli pale shuti la chini la Roberto Firmino
lilipogonga mwamba goli la Villarreal. Wakati mchezo huo ukionekana
kuishia kwa sare tasa Adrian Lopez aliyetokea benchi akafunga goli
akiunganisha pande la Denis Suarez.
Denis Suarez akiwapoteza mahesabu kipa wa Liverpool na beki Kolo Toure na kutoa pande la goli kwa Adrian Lopez
Wachezaji wa Liverpool Milner na Benteke wakishika viuno kuonyesha kukata tamaa baada ya kufungwa goli dakika za majeruhi
Katika mchezo mwingine wa nusu
fainali wa Ligi ya Uropa mabigwa watetezi Sevilla ilitokea nyuma na
kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Shakhtar Donetsk katika mchezo wa
kwanza uliopigwa huko Lviv.
Timu ya Sevilla, ambao ni washindi
wa michuano hiyo mwaka 2014 na mwaka 2015, ilipata goli la kuongoza
mapema kupitia Machin Perez kabla ya Marlos kuipatia Shakhtar Donetsk
goli la kusawazisha.
Taras Stepanenko alipachika goli la
pili kwa Shakhtar Donetsk, hata hivyo penati ya Kevin Gameiro katika
dakika za mwisho iliweza kuipatia Sevilla sare muhimu.
Taras Stepanenko akiwa angani akipiga mpira wa kichwa uliojaa wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni