.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 9 Aprili 2016

MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT) WAFANYIKA DODOMA

Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba, (Kushoto), baada ya kuridhishwa na maelezo ya kina kuhusu huduma na kazi zifanywazo na Mfuko huo katika kutoa mafao ya muda mfupi na fidia ya kudumu kwa Wanyakazi wa Sekta Binafsi na Umma watakaopata ajali na kuumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wazifanyazo mwanzoni mwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa Tanzania (ALAT), ulioanza mjini Dodoma leo Aprili 8, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Juu ya Huduma na Mafao yatakayotolewa na Mfuko hususani fidia ya muda mfupi na fidia ya kudumu kwa Wanyakazi wa Sekta Binafsi na Umma watakaopata ajali na kuumia, kuugua ama kufariki kutoka na kazi. Awali Bw. Mshomba alipata fursa ya kutoa mada kwa wajumbe wa ALAT, kutoka
mikoa mbalimbali kuhusu huduma za Mfuko huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI), Suleiman Jaffo.
                     Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba akiwasilisha mada
                                                   Baadhi ya wajumbe wa ALAT na wageni waalikwa
                                                 Baadhi ya wajumbe wa ALAT na wageni waalikwa
                                      Mmoja wa wajumbe akizungumza kwenye mkutano huo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni