Watu wenye ulemavu wa ngozi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Arusha,Ndg Fadhili Nkurlu.
Arusha.Mkuu
wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu ameitaka halmashauri ya Jiji hilo
kutenga maeneo maulumu ya kuwawezesha wafanyabiashara wenye ulemavu
kufanya shughuli za kujiingizia kipato badala ya kuwatumia mgambo wa
jiji kuwabughudhi.
Nkurlu
ametoa kauli hiyo kwenye mkutano na watu wenye ulemavu uliofanyika kwa
lengo la kutambua changamoto zinazowakabili na namna ya kuzipatia
ufumbuzi na kuwakabidhi kadi ya Bima ya Afya zitakazowawezesha kupata
huduma za afya bure na wategemezi wao watano kwa mwaka .
Pia
watu wenye ulemavu wa ngozi walipewa simu za mikononi 25 zilizotolewa
na kampuni ya Halotel za kuwawezesha kuwasiliana pindi wanapohisi maisha
yao yako hatarini,mafuta maalumu ya kulinda ngozi ,Kofia na Filimbi.
Alisema
miundombinu katika nchi zinazoendelea imekua sio rafiki kwa watu wenye
ulemavu na kukwamisha jitihada zao za kujikomboa na kuwa serikali
itahakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao kama wananchi wengine.
“Najua
zipo asasi zilizoandikishwa kuwasaidia watu wenye ulemavu,lakini sio
zote zinatimiza wajibu huo badala yake zinatumia nafasi hiyo
kujinufaisha tutazichunguza na kuzifuta kabisa zisiwepo kwenye wilaya
hii,”alisema Nkurlu
Ameitaka
halmashauri ya jiji kutumia fedha zinazotengwa kwa makundi maalumu hasa
wenye ulemavu ziwafikie walengwa badala ya kutumika kwa malengo mengine
na kuagiza jiji linapofanya operesheni za kuwaondoa wanaofanya biashara
kwenye maeneo yasiyo rasmi kuwatofautisha na wenye ulemavu.
Kaimu
Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu(Chawata)mkoa wa Arusha(Chawata)Said
Kazigire alisema wanakusudia kufanya sensa ya watu wenye ulemavu ili
kuwa na takwimu sahihi zitakazowasaidia kuwahudumia vyema.
|
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni