Msafara wa Rais John Pombe Magufuli ukiwasili mtaa wa Samora kwenye tawi la benki ya CRDB la Hilland House jijini Dar es salaam.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipokuwa akiondoka katika tawi hilo.
RAIS John Magufuli amezua mjadala baada ya kuvamia tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya “Adamu na Hawa” wala bendera ya Rais.
Tukio hilo lililochukuwa dakika 25, limetokea majira ya asubuhi jijijni Dar es Salaam katika tawi hilo ambalo liko katika makutano ya barabara za Ohio na Samora, bila kutarajiwa.
Mara baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo, makutano ya barabara hizo yalifungwa ndipo Rais aliposhuka kwenye gari na kuingia ndani ya benki hiyo.
Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao waliyokwishaingia.
Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile. Baadhi ya wananchi walisema hawajaona tukio kama lile kwa Marais wote waliyopita.
James Charles, ambaye ni dereva wa taxi, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimarishwa walishituka na mara wakamuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.
“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB, tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja? Hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu. Haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,”alisema Charles.
Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.
“Mimi wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma. Kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,” alisema.
Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni