.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 1 Aprili 2016

MTOTO ALIYEDAIWA MCHAWI NA KUACHWA ILI AFE AREJESHA AFYA YAKE

Mtoto wa miaka miwili wa Nigeria aliyekutwa akiwa amedhofika kiafya kwa minyoo na njaa baada ya kutelekezwa na familia yake ili afe amerejesha afya yake baada ya kuokolewa na msamaria mwema.

Picha ya mtoto huyo akiwa na njaa na utapiamlo akinyweshwa maji ya chupa na mtumishi wa shirika la misaada nchini Nigeria iliwahuzunisha mno watu duniani ilipochapishwa mwezi Januari.

Mtoto huyo wa kiume sasa anaitwa Hope (Matumaini) alitelekezwa na familia yake kutokana na kudhani ni mchawi, alikutwa mitaani na Bi. Anja Ringgren Loven, raia wa Denmark ambaye anaishi Afrika tangu Januari 31. 
Mtoto Hope akinyweshwa maji ya chupa na msamaria mwema baada ya kumkuta mtaani akiwa hivi
                                              Bi. Anja Ringgren akiwa amembeba mtoto Hope 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni