Mtoto wa kike wa miezi minne
amefariki dunia akiwa kwenye ndege angani kutoka Jijini London kwenda
Hong Kong baada ya kupata tatizo lililosababisha ndege hiyo kutua kwa
dharura Kazakhstan.
Wazazi wake waliomba msaada baada ya
kumuona akiwa amepoteza fahamu akiwa kwenye ndege ya shirika la
Cathay Pacific wakati akisafiri kwenda kuwaona ndugu zake nchini
China.
Abiria mmoja ambaye ni muuguzi
alijitokeza kutoa msaada kwa mtoto huyo mchanga, hata hivyo baada ya
ndege hiyo kutua uwanja wa ndege wa Almaty, Kazakhstan ambako
madaktari walikuwepo kumhudumia lakini wakabaini tayari ameshafariki
duni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni