Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kumsimamisha kazi kuanzia leo Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe kutokana na kuingia mikataba tata ambayo imeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 3.
Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo wakati akilizindua daraja la Kigamboni ambalo amependekeza liitwe daraja la Nyerere.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda kuweka hadharani mikataba mibovu iliyoingiwa na Mkurugenzi huyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni