.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 19 Aprili 2016

VICHAKA HATARISHI KATIKA KITUO CHA AFYA BUZURUGA JIJINI MWANZA VYAFYEKWA.

Hali ya Usalama katika Kituo cha Afya cha Kata ya Buzuruga kilichopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza imeimarika, baada ya Wakazi wa Kata hiyo wanaounda Kikundi cha Kijamii cha “Ulipo Tupo” kufyeka vichaka vilivyokuwa katika kituo hicho ambavyo vilikuwa vikitumiwa na
wahalifu kama maficho yao.

Baada ya kufyeka vichaka hivyo jumamosi iliyopita, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Ndaisaba Aron alisema kuwa vichaka hivyo vilikuwa hatarishi kwa wananchi, wagonjwa pamoja na wahudumu wa Afya katika Kituo hicho, kutokana na kupata malalamiko kwamba vibaka walikuwa wakikimbilia katika vichaka hivyo baada ya kufanya uhalifu.

Hidaya Bashiru ambae ni mwanachama wa kikundi hicho pamoja na Sixtus Ijugo ambae ni Katibu, waliwasihi wananchi wengine kuwa na desturi ya kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo katika maeneo mbalimbali kama hospitali, shule nakwingineko kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe.

Diwani wa Kata ya Buzuruga, Richard Machemba, alijumuika na Kikundi hicho kwa ajili ya kufanya usafi katika Kituo hicho ambapo alipongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na wakazi pamoja na vikundi mbalimbali vya maendeleo katika Kata yake ambapo amewasihi wananchi kuendelea kujitoa kwa ajili ya kushirikishughuli za maendeleo.
 
Tazama Picha zaidi hapa chini


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni