Wakati wakubwa zao wakifanya vibaya,
timu ya vijana ya Chelsea imefanikiwa kutwaa kwa mara ya pili
mfululizo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa Vijana baada ya
kuwafunga wenzao wa PSG kwa mabao 2-1.
Beki wa Chelsea Fikayo Tomori
aliipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika 10. Baada ya
kukosa penati katika kipindi cha kwanza PSG ilisawazishwa kupitia kwa
Yakou Meite, hata hivyo baadaye Casey Palmer aliifungia Chelsea goli
la pili.
Vijana wa Chelsea wakiwa na kombe pamoja na medali zao
Casey Palmer akishangilia na wenzake goli la pili alilofunga
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni