Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo jumanne ( 19/04/2016 ) anatarajiwa kulizundua daraja la kisasa la Kigamboni.
Daraja hilo la kisasa kabisa lenye urefu wa mita 680 ni kiunganishi muhimu kwa eneo la Kigamboni na Kurasini wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Kuzinduliwa kwa daraja hilo kutapunguza msongamano wa magari na abiria ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakitumia vivuko kuingia na kutoka Kigamboni.
Wadau mbalimbali wameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, NSSF kwa kusimamia mradi huo hadi kukamilika kwake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni